• HABARI MPYA

  Monday, December 04, 2023

  RAY VANNY ANOGESHA ONYESHO LA UZINDUZI WA ‘VUNA DEILE’

   


  MSANII Raymond Mwakyusa 'Rayvanny', amenogesha uzinduzi wa Promosheni ya ‘Vuna Deile’ iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam.
  Rayvanny alivutia wageni waalikwa walioudhuria uzinduzi huo kutokana na kuimba nyimbo mbalimbali zilizofanya vizuri ndani nan je ya Tanzania.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mratibu wa promosheni hiyo, Nassim Alla, alisema mwaka huu unatamatika na katika msimu huu wa sikukuu jambo kubwa kwa watanzania wote ni ‘Vuna Deile’.
  Vuna Deile ni mchezo wa bahati nasibu ambao una lengo la kubadilisha maisha ya watanzania wote kwa buku tu!
  Alisema kila mtanzania ana nafasi ya kutimiza ndoto zake kwa kucheza Vuna Deile na mchezo huo hauhitaji utaalamu wa aina yoyote zaidi ya kuweka sh. 1,000 tu na utaweza kumiliki gari mpyaa na pia kuvuna mamilioni kila siku.
  "Vuna Deile inapatikana katika mitandao yote ya simu. Kucheza ingia kwenye menyu ya pesa ya mtandao wako, chagua lipa bili, ingiza namba ya kampuni ambayo ni 664455. Weka kumbukumbu namba (namba yako ya simu), weka kiasi shilingi 1,000 (buku tu!), weka namba yako ya siri alafu kamilisha muamala" Alisema.
  Aidha alisema mshiriki atapokea ujumbe wa maneno wenye tokeni namba yako ambapo tokeni hio itaingizwa kwenye ‘spin’ itakayochezeshwa saa 12 jioni kila siku mubashara kupitia chaneli ya ITV na ‘spin’ hiyo itahusisha tokeni namba zote kwa waliocheza saa 24 zilizopita. 
  "Spin zitafanyika kwa awamu mbili, awamu ya kwanza itatoa washindi 10 ambao kila mshindi atajishindia sh. milioni 1, awamu ya pili itatoa mshindi 1 ambaye atajishindia gari mpyaa aina ya Toyota IST”, alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAY VANNY ANOGESHA ONYESHO LA UZINDUZI WA ‘VUNA DEILE’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top