• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  YANGA YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE 1-1 NA AHLY DAR


  WENYEJI, Yanga SC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly katika mchezo wa D Ligi ya Mabingwa Afrika usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Al Ahly walitangulia kwa bao la mshambuliaji wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Percy Muzi Tau dakika ya 86, kabla ya kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacôme Zouzoua kuisawazisha Yanga dakika ya 90 na ushei.
  Al Ahly inafikisha pointi nne na kuendelea kuongoza Kundi D kwa pointi moja zaidi ya wote, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia baada ya mechi mbili za kwanza.
  Mechi zijazo, Yanga itakuwa mgeni wa Medeama Jijini Kumasi Ijumaa ya Desemba 8, wakati Al Ahly watawakaribisha CR Belouizdad Jijini Cairo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE 1-1 NA AHLY DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top