• HABARI MPYA

    Saturday, December 23, 2023

    SIMBA SC YADROO NA KMC 2-2, WAZIRI JUNIOR AMTUNGUA MARA MBILI AYOUB


    TIMU ya Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Mabao yote ya KMC leo yamefungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Waziri Junior Shentembo akimtungua kipa Mmorocco, Ayou Lekred la kwanza lilikuwa la kutangulia dakika ya 31 na la pili la kusawazisha dakika ya 88.
    Kwa upande wao Simba SC mabao yao yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza dakika ya 57 kwa penalti na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke dakika ya 81.
    Simba SC inafikisha pointi 23, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 10 na wote wapo nyuma ya Azam FC inayoongoza kwa pointi zake 31 za mechi 13.
    KMC kwa upande wao baada ya sare ya leo wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nne wakiizidi Singida Fountain Gate pointi moja ambayo sasa inahamia nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC YADROO NA KMC 2-2, WAZIRI JUNIOR AMTUNGUA MARA MBILI AYOUB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top