• HABARI MPYA

  Friday, December 29, 2023

  ARSENAL YAPUNGUZWA KASI, YAGONGWA NYUNDO MBILI NA WEST HAM PALE PALE EMIRATES


  WENYEJI, Arsenal usiku wa jana wamepunguzwa kasi katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-0 na West Ham United Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao yaliyowazamisha The Gunners yalifungwa na Tomas Soucek dakika ya 13 na Konstantinos Mavropanos dakika ya 55 na kwa ushindi huo, Wagonga Nyundo wa London wanafikisha pointi 33 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya sita.
  Kwa upande wao Arsenal baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 40 na kushukia nafasi ya pili sasa wakizidiwa pointi mbili na Liverpool kufuatia wote kucheza mechi 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAPUNGUZWA KASI, YAGONGWA NYUNDO MBILI NA WEST HAM PALE PALE EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top