• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  SIMBA SC MGUU SAWA KUIVAA WYDAD JUMAMOSI MARRAKECH


  KOCHA Mualgeria wa Simba SC, Abdelhak Benchika akiongoza mazoezi ya timu Jijini Marrakech nchini Morocco kujiandaa na mchezo wao wa mwisho mzunguko wa kwanza Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Wydad Casablanca Jumamosi Saa 4:00 usiku Uwanja wa Marrakech.
  Mechi mbili za awali, Simba SC ilitoa sare ya 1-1 na ASEC Mimosas ya Ivory Coast Novemba 25 Jijini Dar es Salaam na suluhu (0-0) na Jwaneng Galaxy Desemba 2 Jijini Francistown, Botswana.
  Kwa upande wao Wydad Athletic walifungwa 1-0 mfululizo mara mbili, nyumbani Marrakech Novemba 25 na Jwaneng Galaxy na ugenini Desemba 2 mbele ya ASEC Mimosas Uwanja wa Félix Houphouët-Boigny Jijini Abidjan. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC MGUU SAWA KUIVAA WYDAD JUMAMOSI MARRAKECH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top