• HABARI MPYA

  Friday, December 22, 2023

  KAGERA SUGAR YATEMANA NA MECKY MEXIME KWA MARIDHIANO YA WOTE


  TIMU ya Kagera Sugar imeachana na Kocha wake Mkuu, Mecky Mexime Kianga pamoja na Kocha wa Fiziki, Francis Mkanula kwa makubaliano ya pande zote mbili.
  Hatua hiyo inakuja siku moja baada ya Kagera Sugar kuchapwa mabao 4-0 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa nyumbani, Kaitaba mjini Bukoba.
  Kipigo hicho cha tatu mfululizo wakitoka kufungwa mechi mbili ugenini, 1-0 na Coastal Unión Desemba 9 na 3-0 dhidi ya Simba SC kinaiporomosha Kagera Sugar hadi nafasi ya 14 ikibaki na pointi zake 13 za mechi 13.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YATEMANA NA MECKY MEXIME KWA MARIDHIANO YA WOTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top