• HABARI MPYA

  Sunday, December 10, 2023

  LAKERS BINGWA WA MICHUANO YA NBA IN-SEASON TOURNAMENT 2023


  TIMU ya Los Angeles Lakers imefanikiwa kutwaa taji jipya la NBA In-Season Tournament baada ya ushindi wa pointi 123-109 dhidi ya Indiana Pacers Alfajiri ya leo ukumbi wa T-Mobile Arena Jijini Las Vegas.
  Nyota na gwiji wa Los Angeles Lakers, LeBron James voted alichaguliwa Mchezaji Bora  (MVP) wa Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu.
  Katika ushindi huo, Anthony Davis aliongoza kufunga pointi,  41 na rebounds 20, akifuatiwa na Austin Reaves pointi 28, LeBron James pointi 24 na rebounds 11 na D’Angelo Russell pointi 13.
  Kwa ushindi huo, kila mchezaji wa Lakers atapatiwa donge nono la dola za Kimarekani 500,000, wakati Indiana Pacers kila mmoja atapata dola 200,000 kwa kufika Fainali - huku Milwaukee Bucks na New Orleans Pelicans zilizoishia Nusu Fainali wakipata dola 100,000 kila mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LAKERS BINGWA WA MICHUANO YA NBA IN-SEASON TOURNAMENT 2023 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top