• HABARI MPYA

  Tuesday, December 12, 2023

  SIMBA QUEENS WABEBA NGAO, YANGA PRINCESS WA TATU


  TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii kuelekea msimu mpya wa Ligi ya Wanawake Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT Queens kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  JKT Queens walitangulia kwa bao la Stumai Abdallah dakika ya 15, kabla ya Danai Bhobho kuisawazishia Simba Queens dakika ya 24 mabao yote yakizalishwa na mipira ya kona.
  Katika mchezo uliotangulia kusaka mshindi wa tatu, Yanga Princess waliifunga Fountain Gate Princess kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 hapo hapo Azam Complex.
  Ikumbukwe JKT Queens waliitoa Fountain Gate Princess kwa kuichapa mabao 5-0, wakati Simba Queens iliitoa Yanga Princess kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 katika mechi za Nusu Fainali Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS WABEBA NGAO, YANGA PRINCESS WA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top