• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  BARA YAITOA ZANZIBAR KWA 'SHERIA YA KADI ZA NJANO' CECAFA U18


  LICHA ya sare ya kufungana bao 1-1 na ndugu zao, Zanzibar leo katika mchezo wa mwisho wa Kundi B michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 18 Afrika Mashariki na Kati (CECAFA U18) Uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega nchini Kenya, Tanzania Bara imefanikiwa kwenda Nusu Fainali.
  Baada ya sare hiyo timu hizo zikamaliza zikiwa zimefungana kwa pointi, nne kila moja na wastani wa mabao na ndipo Kamati ya Mashindano hayo ya CECAFA ilipoamua Bara iende Nusu Fainali kwa kigezo cha mchezo wa kiungwana kwa sababu wachezaji wake wameonyeshwa kadi za njano nne tu, huku Zanzibar wakiwa wana moja zaidi, tano.
  Uganda imefuzu kama kinara wa Kundi B kwa pointi zake sita na itakutana na mshindi wa pili wa Kundi A, Rwanda wakati Bara watamenyana na wenyeji, Kenya wiki ijayo huko Kisumu.
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARA YAITOA ZANZIBAR KWA 'SHERIA YA KADI ZA NJANO' CECAFA U18 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top