• HABARI MPYA

    Saturday, December 23, 2023

    AL AHLY WAIHESHIMISHA AFRIKA KLABU BINGWA YA DUNIA


    TIMU ya Al Ahly ya Misri jana ilifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu katika Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Urawa Red Diamonds ya Japan Uwanja wa Prince Abdullah al-Faisal Jijini Jeddah, Saudi Arabia.
    Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Yasser Ibrahim dakika ya 19, Percy Tau dakika ya 25, Yoshio Koizumi aliyejifunga dakika ya 60 na Ali Maaloul dakika ya 90, wakati ya Urawa Red Diamonds yamefungwa na José Kanté dakika ya 43 Alexander Scholz kwa penalti dakika ya 54. 
    Ni Manchester City mabingwa wapya wa Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fluminense ya Brazil jana Uwanja wa King Abdullah Sports City Jijini Jeddah, Saudi Arabia.
    Mabao ya Manchester City yalifungwa na Julian Alvarez mawili dakika ya kwanza na 88, Nino aliyejifunga dakika ya 27 na Phil Foden dakika ya 72.
    Hilo linakuwa taji la tano mwaka huu kwa kocha Mspaniola, Pep Guardiola baada ya awali kubeba mataji ya Ligi Kuu England, Kombe la FA, Ligi ya Mabingwa Ulaya na UEFA Super Cup.
    Kwa kutwaa Kombe hilo, Manchester City imejinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 5, huku Fluminense wakipata Dola Milioni 4 kwa kushika nafasi ya pili, Al Ahly Dola Milioni 2.5 kwa kushika nafasi ya tatu na Urawa Red Diamonds Dola Milioni 2 kwa kumaliza ya nne.
    León ya Mexico na Al Ittihad ya Saudi Arabia zilizoshia Raundi ya Pili kila moja imepata Dola Milioni 1, wakati Auckland City ya New Zealand iliyofungwa na Al Ittihad katika Raundi ya kwanza  imerejea nyumbani na Dola 500,000.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AL AHLY WAIHESHIMISHA AFRIKA KLABU BINGWA YA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top