• HABARI MPYA

  Monday, December 25, 2023

  BARA WALIVYOONDOKA DAR KUIFUATA ZANZÍBAR MECHI JUMATANO


  WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania Bara wakiwa Bandarini kwa safari ya Zanzíbar kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Zanzíbar Heroes Jumatano.
  Kocha Mualgeria, Adel Amrouche anataka kutumia mchezo huo kuteua kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwakani nchini Ivory Coast.
  Lakini katika majina ya awali 53 yaliyotumwa makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) jina la Mzize limo na orodha hiyo itachujwa hadi kubaki wachezaji 27, lakini ni 23 tu watakaoruhusiwa kucheza AFCON zitakazofanyika kuanzia Januari 13 hadi Februari 11 mwakani nchini Ivory Coast.
  Taifa Stars imepangwa Kundi F pamoja na Morocco, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
  Kwa Taifa Stars hizo Zita kuwa Fainali za tatu za AFCON kucheza baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri, kote wakitolewa hatua ya makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARA WALIVYOONDOKA DAR KUIFUATA ZANZÍBAR MECHI JUMATANO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top