• HABARI MPYA

  Tuesday, December 19, 2023

  MTIBWA SUGAR YAICHAPA MASHUJAA 2-1 MANUNGU

   

  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro. 
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na kiungo Seif Abdallah Karihe dakika ya 23 na mshambuliaji Matheo Anthony Simon dakika ya 73, huku bao pekee la Mashujaa likifungwa na mshambuliaji Adam Adam dakika ya 41. 
  Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi nane katika mchezo wa 14, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16 ikizidiwa pointi moja na Mashujaa FC iliyocheza mechi 12 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAICHAPA MASHUJAA 2-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top