• HABARI MPYA

  Monday, December 11, 2023

  AZAM FC YAICHAPA JKT TANZANIA 2-1 NA KUZIDI ‘KUPOTELEA’ KILELENI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Nahodha Sospeter Bajana dakika ya kwanza na Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 84, huku bao pekee la JKT Tanzania likifungwa na Najim Magulu dakika ya 37.
  Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 28 katika mchezo wa 12 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi tatu mkononi.
  Kwa upande wao JKT Tanzania baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 16 za mechi 13 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA JKT TANZANIA 2-1 NA KUZIDI ‘KUPOTELEA’ KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top