• HABARI MPYA

  Monday, December 11, 2023

  SINGIDA YATOA DROO 0-0 NA KMC KARATU


  TIMU ya Singida Fountain Gate imelazimishwa sare ya bila mabao na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Black Rhino Academy uliopo Karatu Jijini Arusha.
  Kwa sare hiyo kila timu zote zinafikisha pointi 20 na Singida Fountain Gate wanabaki nafasi ya nne wakiizidi tu wastani wa mabao KMC inayobaki nafasi ya tano pia.
  Wakati huo huo: Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeipa adhabu nyingine Singida Fountain Gate kutofanya usajili hadi itakapomlipa kiungo Mbrazil, Rodrigo Figueiredo Carvalho.
  Tayari Singida Fountain Gate wana adhabu kama hiyo kwa madai ya beki Muivory Coast, Serge Wawa na hawataruhusiwa kusajili hadi wamalizane na wachezaji hao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA YATOA DROO 0-0 NA KMC KARATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top