• HABARI MPYA

    Sunday, December 24, 2023

    GEITA INSTITUTE WAIBUKA NA UBINGWA KANYASU CUP


    MICHUANO ya Ligi Daraja la Nne ngazi ya wilaya ya Geita kwa mwaka 2023 maarufuka kama KANYASU CUP  imetamatika kwa Geita Institute kuibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya kuichapa timu ya  Shadow Boys Fc bao moja kwa 1 kwa yai .
    Timu ya Geita Institute  imeibuka na ubingwa huo kwenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo ulipigwa katika uwanja wa GGML mjini Geita na kujinyakulia   kitita cha shilingi milioni 1 kikombe, mpira mmoja  na jezi huku mshindi wa pili timu ya shadow boys fc wakiibuka na shilingi laki tano jezi na mpira na mshindi wa tatu timu ya mgusu  fc akiambulia shilingi laki tatu.
     Msemaji msaidizi wa timu ya  Geita institute Willbert Ngasa alisema kuwa kwa ushindi huo wamejipanga kutinga kikamilifu kwenye michuano ya lingi daraja la tatu ngazi ya mkoa huo .
    Alisema kuwa kitendo cha mbunge huyo kudhamini ligi ya ngazi ya chini kiwe funzo kwa wadau wengine wa soka pamoja na wabunge wengine kwa kuwa huko ndiko kuna vijana wengi wenye vipaji waliofichika .
     Makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Geita GEDFA  Vallence Ibrahim alisema kuwa udhamini  wa ofisi ya Mbunge wa jimbo la Geita mjini katika michuano hiyo umekuwa chachu katika kuibua vipaji vya  soka kwa vijana Wilayani humo.


    Alisema kuwa ofisi ya mbunge huyo inadhamini michuano hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu  huu ukiwa ni mwaka pili wa udhamini huo ambapo kila mwaka zaidi ya shilingi milioni 15 hutumika ikiwemo kugharamika jezi kwa shiriki, matibabu   kwa kipindi chote cha michuano hiyo pamoja na malipo ya waamuzi .
     Aidha mbunge wa jimbo la Geita mjini Costantine Kanyasu akikabidhi zawadi kwa washindi alisema kuwa atahakikisha wanaboresha mazingira ya viwanja vya michezo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio.
    “Tuna mazungumzo na GGML uwanja huu uweze kuwekewa nyasi bandia na uzio ili vijana waweze kutimiza kiu yao na chama cha soko kiweze kukusanya mapato walau kidogo wakati wa lingi “alisema mbunge Kanyasu .
    Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi septemba 10 mwaka huu katika uwanja wa shule ya sekondari ya Kalangalala mjini Geita ikishirikisha timu 16 za Wilayani humo.
    (Imeandikwa na Alphonce  Kabilondo kutoka Geita)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GEITA INSTITUTE WAIBUKA NA UBINGWA KANYASU CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top