• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-1 NA KUTANUA UONGOZI ENGLAND


  WENYEJI, Arsenal FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukato Saka dakika ya sita na Martin Odegaard dakika ya13, wakati bao la Wolves limefungwa na Matheus Cunha dakika ya 86.
  Kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 33 katika mchezo wa 14 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi nne zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City ambao wana mechi moja mkononi, wakati Wolves inabaki na pointi zake 15 za mechi 14 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA WOLVES 2-1 NA KUTANUA UONGOZI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top