• HABARI MPYA

  Thursday, December 21, 2023

  LIVERPOOL YATINGA NUSU FAINALI CARABAO CUP KWA USHINDI WA 5-1


  WENYEJI, Liverpool FC jana wametinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England kwa ushindi wa kishindo wa mabao 5-1 dhidi ya West Ham United Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Dominik Szoboszlai dakika ya 28, Curtis Jones dakika ya 56 na 84, Cody Gakpo dakika ya 71 na Mohamed Salah dakika ya 82, huku la West Ham likifungwa na Jarrod Bowen dakika ya 77.
  Sasa Liverpool itakutana na Fulham iliyoitoa Everton juzi kwa penalti 7-6 baada ya sare ya 1-1, wakati Nusu nyingine ni katí ya Chelsea na Middlesbrough.
  Chelsea iliitoa Newcastle United kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Middlesbrough iliitandika Port Vale 3-0 katika mechi za juzi za Robó Fainali ya michuano hiyo inayojulikana kama Carabao Cup.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATINGA NUSU FAINALI CARABAO CUP KWA USHINDI WA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top