• HABARI MPYA

    Thursday, December 14, 2023

    MANCHESTER CITY YAMALIZA NA USHINDI WA 3-2 BELGRADE


    MABINGWA watetezi, Manchester City wamekamilisha mechi zao za Kundi G kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wenyeji, Red Star Belgrade usiku wa jana Uwanja wa Rajko Mitić Jijini Belgrade, Serbia.
    Mabao ya Manchester City yamefungwa na chipukizi Micah Hamilton dakika ya 19 na Oscar Bobb dakika ya 62 huku Kalvin Phillips akifunga la ushindi kwa penalti dakika ya 85.
    Kwa upande wao wenyeji, Red Star Belgrade mabao yao yalifungwa na Hwang In-Beom dakika ya 76 na Aleksandar Katai dakika ya 90 na ushei.
    Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 18, mbele ya RB Leipzig iliyomaliza na pointi 12 baada ya jana kuifunga 2-1 Young Boys inayomaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi nne na Red Star Belgrade wenye pointi moja wameshika mkia.
    Manchester City na RB Leipzig zimefuzu Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya huku Young Boys wakihamia Europa League wakati Red Star safari yao inaishia hapa kwenye msimu huu wa michuano ya Ulaya ngazi ya klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAMALIZA NA USHINDI WA 3-2 BELGRADE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top