• HABARI MPYA

  Wednesday, December 06, 2023

  BETIKA YALETA PROMO KUPELEKA MASHABIKI KUSHUHUDIA AFCON IVORY COAST


  KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Betika kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, wamezindua Promosheni maalum ya kupeleka washindi wake kwenye michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Ivory Coast. 
  Katika michuano hiyo itakayoanza Januari 13 hadi Februari 11 mwakani nchini Ivory Coast, Betika kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, itapeleka washindi wa promo hiyo kwenye AFCON ya mwakani kuishuhudia timu yao ya Taifa, Taifa Stars ikicheza mechi zake za Kundi F.
  Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa, alisema watanzania wakaobashiriki kupitia Betika kwa kushirikiana na Tigo wataenda nchini Ivory Coast kushuhudia mechi za Taifa Stars.
  Alisema sasa wamekuja na promosheni hiyo baada ya kupita nyingine kubwa ambayo jumla ya mashabiki 400 kutoka mikoa mbalimbali walishuhudia mechi za watani wa jadi za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.
  Rugambwa alisema promosheni hiyo iliyopewa jina la ‘Twende Zetu Ivory Coast,KI VIP’ imenza rasmi na droo kubwa itafanyika Januari 2, kwa washindi 6 watapatikana ambapo washindi watapata huduma zote, kuanzia hapa nchini na hadi wakiwa nchini humo.
  Alisema licha ya kuwepo kwa safari hiyo ya Ivory Coast, kuna zawadi mbalimbali za washindi ambapo televisheni nchi 70 kutoka Kampuni ya Hisense kila wiki kwa washindi wawili, zikiwa zimeambatana na king’amuzi, vikiwa vimeunganishwa na vifurishi vya mwezi mzima kutoka Kampuni ya Dstv na mamilioni kushindaniwa.
  Kwa upande wa Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Fabian Feliciana, alisema wao ni miongoni mwa wadau wakubwa wa soka wameona ni vizuri kushirikiana na Betika kuhakikisha washiriki wanacheza na kupata safari ya kwenda kushuhudia timu ya Taifa ikipeperusha bendera nchini Ivory Coast.
  ‘Tigo Pesa na Betika tunakwambia ‘Twende Zetu Ivory Coast,KI VIP’ ili uweze kujishindia safari hiyo weka pesa tigo pesa alafu ingia kwenye menyu ya *150*01,alafu utaingia namba 4 na kuweka no.545454, cheza Betika uende Ivory Coast KiVIP zaidi,” alisema Felician.                                                                     Katika michuano hiyo 24 zitachuana kuwania kuombe hilo ambapo Tanzania hii ni mara ya tatu kushiriki fainali hizo, Tanzania ipo pamoja na Morocco, DR Congo na Zambia, makundi mengin  (A) lina wenyeji  Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, naGuinea-Bissau, Kundi( B)  zipo Misri, Ghana, Cape Verde na  Msumbiji.
  Wakati  Kundi (C) zipo  Senegal, Cameroon, Guinea na  The Gambia, Kundi (D) Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola na Kundi E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na  Namibia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BETIKA YALETA PROMO KUPELEKA MASHABIKI KUSHUHUDIA AFCON IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top