• HABARI MPYA

  Sunday, December 31, 2023

  AZAM FC YASAJILI KIPA WA TIMU YA TAIFA YA SUDAN KWA MKOPO


  KLABU ya Azam FC imemsajili kipa wa Kimataifa wa Sudan, Mohamed Mustafa kwa mkopo wa miezi sita kutoka El Merreikh ya kwao, Omdurman.
  Mohamed Mustafa (27) ambaye pia anadakia timu ya taifa ya Sudan, anajiunga na Azam FC kutoka Al-Ahli ya Atbara alipokuwa anacheza kwa mkopo pia tangu mwaka 2018.
  Mustafa alijiunga na Merreikh Omdurman mwaka 2014 akitokea Merreikh Al-Fasher aliyoanza kuidakia mwaka 2011, kabla ya mwaka 2017 kupelekwa kwa mkopo Al-Merrikh SC ya Nyala na baadaye Al-Ahli Atbara.
  Huyo anakuwa kipa wa tatu wa kigeni kwenye kikosi cha Azam FC baada ya Mcomoro, Ali Ahamada (32) na Mghana Iddrisu Abdulai (26).
  Baada ya kuumia mnfululizo kwa makipa hao wa kigeni mapema Desemba, Azam FC ikawa inamtumia kipa wa tatu, Zuberi Foba Masoud (21) kwenye mechi zake ambaye alifanya vizuri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YASAJILI KIPA WA TIMU YA TAIFA YA SUDAN KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top