• HABARI MPYA

  Thursday, December 28, 2023

  MANCHESTER CITY YAICHAPA EVERTON 3-1 GOODISON PARK


  MABINGWA watetezi, Manchester City jana wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Everton katika mchezo wa Kigi Kuu England Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool.

  Haukuwa ushindi wa mteremko, kwani Manchester City walilazimika kutoka nyuma baada ya Jack Harrison kuanza kuifungia Everton dakika ya 29. 
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Phil Foden dakika ya 53, Julian Alvarez kwa penalti dakika ya 64 na Bernardo Silva dakika ya 86 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 37 katika mchezo wa 18 na kupanda nafasi ya nne, wakati Everton inabaki na pointi zake 16 za mechi ya 19 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAICHAPA EVERTON 3-1 GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top