• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2023

  SINGIDA YAITUPA NJE ARUSHA CITY AZAM FEDERATION CUP


  TIMU ya Singida Fountain Gate imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Arusha City leo Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu Jijini Arusha.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yamefungwa na kiungo mzawa Yussuf Kagoma dakika ya 10 na Wakenya, mshambuliaji Elvis Rupia dakika ya 29 na kiungo Duke Abuya dakika ya 50.
  Mechi nyingine za leo Hatua ya Timu 64 Gunners FC imewatoa wenyeji, Ken Gold kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Transit Camp imeitoa Airport FC kwa mabao 2-0 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Rhino Rangers imewatoa Cosmopolitan kwa mabao 2-1 Uwanja wa TFF Kigamboni, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA YAITUPA NJE ARUSHA CITY AZAM FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top