• HABARI MPYA

  Monday, December 04, 2023

  TRENT ALEXANDER-ARNOLD AIPA USHINDI LIVERPOOL


  WENYEJI, Liverpool jana wamepata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Fulham katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na kipa Bernd Leno aliyejifunga akijaribu kuokoa mpira wa adhabu wa Trent Alexander-Arnold dakika ya 20, ambaye ndiye alifunga bao la nne na la ushindi dakika ya 88, mengine Alexis Mac Allister dakika ya 38 na Wataru Endo dakika ya 87.
  Mabao ya Fulham yamefungwa na Harry Wilson dakika ya 24, Kenny Joelle Tete dakika ya 45 na Bobby Armani De Cordova-Reid dakika ya 80.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 31 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal wakati Fulham inabaki na pointi zake 15 nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi 14.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TRENT ALEXANDER-ARNOLD AIPA USHINDI LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top