• HABARI MPYA

  Saturday, December 30, 2023

  MAN CITY YAWACHAPA VIBONDE SHEFFIELD UNITED 2-0 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Rodri dakika ya 14 na Julian Alvarez dakika ya 61 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 40 na kusogea nafasi ya tatu, wakiizidi tu wastani wa mabao Arsenal baada ya wote kucheza mechi 19, wakati Sheffield United inabaki na pointi zake tisa mkiani baada ya kucheza mechi 20 kwenye Ligi ya timu 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAWACHAPA VIBONDE SHEFFIELD UNITED 2-0 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top