• HABARI MPYA

  Sunday, December 31, 2023

  KIPRE JUNIOR MCHEZAJI BORA, BRUNO KOCHA BORA LIGI KUU DESEMBA


  WINGA wa Azam FC, Zenón Kipre Emmanuel Junior amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Desemba 2023 akiwashinda Prince Dube Mpumelelo anayecheza naye timu moja na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki wa Yanga.
  Pamoja naye, Kocha wa timu hiyo, Mfaransa Bruno Ferry ameshinda Tuzo ya Kocha Bora wa Mwezi huo dhidi ya Muargentina Miguel Gamondi wa Yanga na Ahmad Ally wa Tanzania Prisons.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIPRE JUNIOR MCHEZAJI BORA, BRUNO KOCHA BORA LIGI KUU DESEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top