• HABARI MPYA

  Sunday, December 17, 2023

  AZAM FC YAICHAPA ALLIANCE 2-1 NA KUSONGA MBELE ASFC


  TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Alliance FC ya Mwanza leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Msenegal, Alasane Diao dakika ya 48 na kiungo Mghana, James Akaminko dakika ya 56, wakati bao pekee la Alliance FC limefungwa na Eric Mwita dakika ya 90 na ushei.
  Mechi nyingine za Hatua ya timu 64 leo, KMC imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya ACÁ Eagle baada ya sare ya bila kufungana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Nayo Mbeya City imeichapa African Lyon 2-0 Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Mabao FC imewang’oa wenyeji, Copco kwa kuwachapa 2-1 Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza, Mkwajuni FC imewatoa wenyeji, Ruvu Shooting kwa 1-0 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na TMA FC imeitandika Sharp Lion 7-2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA ALLIANCE 2-1 NA KUSONGA MBELE ASFC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top