• HABARI MPYA

  Saturday, December 30, 2023

  MAN UNITED KAMA KAWAIDA YAO, WAMEPIGWA 2-1 THE CITY


  WENYEJI, Nottingham Forest wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa The City Ground mjini Nottingham, Nottinghamshire.
  Mabao ya Nottingham Forest yamefungwa na Nicolás Domínguez dakika ya 64 na Morgan Gibbs-White dakika ya 82, wakati bao pekee la Manchester United limefungwa na Marcus Rashford dakika y 78.
  Kwa ushindi huo, Nottingham Forest inafikisha pointi 20 na kusogea nafasi ya 15, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 31 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED KAMA KAWAIDA YAO, WAMEPIGWA 2-1 THE CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top