• HABARI MPYA

  Monday, December 04, 2023

  IHEFU YAAMBULIA SULUHU KWA PRISONS MBARALI


  WAKIWA Uwanja wa nyumbani, Highland Estate, Mbarali - Ihefu wamelazimishwa sare ya bila mabao na ndugu zao, Tanzania Prisons, zote za Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 10, ingawa inabaki nafasi ya 14, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi 11 na yenyewe inabaki nafasi ya 13 kwenye Ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 12.
  Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitateremka moja kwa moja na mbili zitamenyana zenyewe nyumbani na ugenini itakayoshinda itabaki Ligi Kuu na itakayofungwa itakwenda kucheza na timu ya Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAAMBULIA SULUHU KWA PRISONS MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top