• HABARI MPYA

  Friday, December 08, 2023

  YANGA SC YATOA SARE NA MEDEAMA SC 1-1 KUMASI


  TIMU ya Yanga imekamilisha mechi zake tatu za mzunguko wa kwanza wa mechi zake za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika bila ushindi baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Medeama SC usiku huu Uwanja wa Baba Yara Jijini Kumasi nchini Ghana.
  Mshambuliaji Jonathan Sowah alianza kuifungia Medeama kwa penalti dakika ya 27, kabla ya kiungo Muivory Coast, Pacome Zouazoua kuisawazishia Yanga dakika ya 36.
  Mchezo mwingine wa Kundi D leo, Al Ahly imelazimishwa sare ya bila mabao na CR Belouizdad ya Algeria usiku huu pia Uwanja wa Borg El Arab Jijini Alexandria, Misri.
  Al Ahly inaendelea kuongoza Kundi D kwa pointi zake tano, ikifuatiwa na CR Belouizdad yenye pointi nne sawa na Medeama, wakati Yanga yenye pointi mbili inashika mkia.
  Mechi zijazo, Yanga watawakaribisha Medeama Jijini Dar es Salaam Jumatano ya Desemba 20, wakati Al Ahly watakuwa wageni wa CR Belouizdad Jijini Algiers Jumanne ya Desemba 19.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATOA SARE NA MEDEAMA SC 1-1 KUMASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top