• HABARI MPYA

  Sunday, December 24, 2023

  JOSHUA ASHINDA TKO, WILDER APIGWA 'KAMA BEGI' SAUDI ARABIA


  BONDIA Muingereza mwenye asili ya Nigeria, Anthony Joshua usiku wa jana ameshinda kwa Technical Knockout (TKO)  Otto Wallin wa Sweden ambaye alijiuzulu ulingoni raundi ya tano kufuatia wasaidizi wake kurusha taulo ulingoni katika pambano lisilo la ubingwa la uzito wa juu ukumbi wa Kingdom Arena, Jijini Riyadh, Saudi Arabia.
  Naye Mmarekani, Deontay Wilder alipoteza pambano la kuwania mataji ya WBC International WBO Inter-Continental baada ya kushindwa na Joseph Parker wa New Zealand kwa pointi za majaji wote, Michael Alexander akitoa 118-111, Steve Gray 120-108 na John Latham 118-110.
  Matokeo hayo yanamaanisha uwezekano wa pambano baina ya Joshua na Deontay Wilder kutokea ni mdogo sasa na Promota Eddie Hearn amesema kwamba sasa bondia wake atazipiga na n Filip Hrgovic wa Croatia kuwania taji la IBF la dunia ambalo lipo wazi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOSHUA ASHINDA TKO, WILDER APIGWA 'KAMA BEGI' SAUDI ARABIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top