• HABARI MPYA

    Sunday, December 17, 2023

    ARSENAL YAITWANGA BRIGHTON 2-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND


    WENYEJI, Arsenal wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
    Mabao ya The Gunners yamefungwa na Gabriel Jesus dakika ya 53 na Kai Havertz dakika ya 87 na kwa ushindi huo Arsenal inafikisha pointi 39 na kurejea kileleni mwa Ligi, wakati Brighton & Hove Albion inabaki na pointi zake 26 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 19.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAITWANGA BRIGHTON 2-0 NA KUREJEA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top