• HABARI MPYA

  Monday, December 04, 2023

  MAN CITY YADHIBITIWA PALE PALE ETIHAD, 3-3 NA SPURS


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 3-3 na Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Son Heung-Min alijifunga dakika ya tisa, Philip Foden dakika ya 31 na Jack Grealish dakika ya 81.
  Mabao ya Tottenham Hotspur yamefungwa na Son Heung-Min dakika ya sita, Giovani Lo Celso dakika ya 69 na Dejan Kulusevski dakika ya 90.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City wanajiongezea pointi moja na kufikisha 30, hivyo wanashuka hadi nafasi ya tatu, wakati Tottenham Hotspur imefikisha pointi 27 ikihamia nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YADHIBITIWA PALE PALE ETIHAD, 3-3 NA SPURS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top