• HABARI MPYA

  Sunday, December 24, 2023

  WOLVES YAICHAPA CHELSEA 2-1 MOLINEUX


  WENYEJI, Wolverhampton Wanderers wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Mabao ya Wolves yamefungwa na Mario Lemina dakika ya 51 na Matt Doherty dakika ya 90 na ushei, kabla ya Christopher Nkunku kuifungia Chelsea bao la kufutia machozi dakika za mwisho wa muda ziada.
  Kwa ushindi huo, Wolves wanafikisha pointi 22, sawa na Chelsea lakini wanabaki nafasi ya 11 wakizidiwa wastani wa mabao na The Blues baada ya wote kucheza mechi 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WOLVES YAICHAPA CHELSEA 2-1 MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top