• HABARI MPYA

  Saturday, December 30, 2023

  SINGIDA YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, YAUA 4-1


  TIMU ya Singida Fountain Gate jana imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024 baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, JKU katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa New Amani Complex, Zanzibar.
  Mabao ya Singida Fountain Gate yalifungwa na washambuliaji, Mkenya Elvis Rupia mawili dakika ya 16 na 48, Mnyarwanda Meddie Kagere dakika ya 80 na Mkongo Francy Kazadi dakika ya 86, wakati la JKU limefungwa na Saleh Masoud Abdallah dakika ya 61 kwa penalti.
  Mchezo uliotangulia jana wa Kundi C, KVZ iliichapa Jamhuri 2-0, mabao ya Akram Mhina dakika ya nane na 53.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA YAANZA NA MOTO KOMBE LA MAPINDUZI, YAUA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top