• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA SHEFFIELD UNITED 2-0 BRAMALL LANE


  TIMU ya Liverpool FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Sheffield United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Bramall Lane mjini Sheffield.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na beki Mholanzi, Virgil van Dijk dakika ya 37 na kiungo wa Kimataifa wa Hungary, Dominik Szoboszlai dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 34, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal baada ya wote kucheza mechi 15, wakati Sheffield United inaendelea kushika mkia na pointi zake tano za mechi 15 pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA SHEFFIELD UNITED 2-0 BRAMALL LANE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top