• HABARI MPYA

  Sunday, March 17, 2019

  ZIDANE AREJEA NA MGUU MZURI, REAL YAICHAPA CELTA VIGO 2-0

  Gareth Bale akishangilia baada ya kuifungia bao la pili Real Madrid dakika ya 77 kufuatia Isco kufunga la kwanza dakika ya 62 ikiilaza Celta Vigo 2-0 katika mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Bernabeu, Zinadine Zidane akirejea na mguu mzuri kwa ushindi katika mchezo wake wa kwanza baada ya kupewa tena mikoba ya kuionoa timu hiyo. Kwa ushndi huo, Real Madrid inafikisha pointi 54 katika mchezo wa 28, ikiendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid yenye pointi 56 za mechi 28 pia na Barcelona pointi 63 mechi 27 
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE AREJEA NA MGUU MZURI, REAL YAICHAPA CELTA VIGO 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top