• HABARI MPYA

  Monday, December 18, 2023

  DODOMA JIJI YAICHAPA IHEFU SC 1-0 JAMHURI


  WENYEJI  Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Bao hilo pekee la Walima Zabibu limefungwa na Yassin Mgaza dakika ya 55 na kwa ushindi huo, wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya saba, wakati Ihefu SC inabaki na pointi zake 13 za mechi 14 nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA IHEFU SC 1-0 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top