• HABARI MPYA

  Saturday, December 23, 2023

  WEST HAM YAIGONGA NYUNDO MBILI MAN UNITED


  TIMU ya West Ham United imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London.
  Mabao ya Wagonga Nyundo hao wa London yamefungwa na Jarrod Bowen dakika ya 72 na Mohammed Kudus dakika ya 78.
  Kwa ushindi huo West Ham wanafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya sita, wakati Manchester United inabaki na pointi zake 28 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 18. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM YAIGONGA NYUNDO MBILI MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top