• HABARI MPYA

  Wednesday, December 20, 2023

  YANGA YAITANDIKA MEDEAMA 3-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBÓ FAINALI


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wamefufua matumaini ya kwenda Robó Fainali ya Ligi Mabingwa Afrika kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Medeama ya Ghana jioni ya leo Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 33, mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 61 na kiungo mzawa, Mudathir Yahya Abbas dakika ya 66.
  Pongezi kwa kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliyeokoa mkwaju wa penalti wa Jonathan Sowah dakika ya 55 kufuatia mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Ghana huyo kuchezewa rafu na mlinzi na Nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto. 
  Medeama ilimaliza pungufu baada ya Sowah kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya pili, nyuma ya mabingwa watetezi, Al Ahly wanaoogoza kwa wastani wa mabao wakiwa na mechi moja mkononi.
  Medeama inashukia nafasi ya tatu ikibaki na pointi zake nne za mechi nne pia nyuma ya CR Belouizdad ya Algeria yenye pointi nne pia na wastani zaidi wa mabao wakiwa na mechi moja mkononi pia.
  Mechi zijazo, Yanga watakuwa wenyeji wa CR Belouizdad Februari 23, kabla ya kwenda kumalizia mechi za Kundi D Jijini Cairo dhidi ya Al Ahly Machi 1 mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAITANDIKA MEDEAMA 3-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBÓ FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top