• HABARI MPYA

  Saturday, December 16, 2023

  MAN CITY YANG'ANG'ANIWA NA CRYSTAL PALACE, SARE 2-2 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City  wamelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Manchester City ilionekana kuondoka na ushindi baada ya kutangulia kwa mabao ya Jack Grealish dakika ya 24 na Rico Lewis dakika ya 54, kabla ya Crystal Palace kusawazisha kupitia kwa Jean-Philippe Mateta dakika ya 76 na Michael Olise kwa penalti dakika ya 90 na ushei.
  Kwa sare hiyo, Manchester City wanafikisha pointi 34, ingawa wanabaki nafasi ya nne, wakati Crystal Palace inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 17 nafasi ya 15.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YANG'ANG'ANIWA NA CRYSTAL PALACE, SARE 2-2 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top