• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2023

  BENO KAKOLANYA AFUNGIWA NA FAINI JUU KWA MATUSI NA UGOMVI


  KIPA wa Singida Fountain Gate, Benno David Kakolanya amefungiwa mechi tatu na kutozwa Faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kujaribu kumshambulia kiongozi wa Coastal Union, Juma Kindo na kumtolea maneno machafu wakati wa mchezo baina ya timu hizo Novemba 27 Uwanja wa LITI, Singida.
  Katika mchezo huo ambao Singida Fountain Gate walishinda 2-1, pia kama timu wametozwa Faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kuingia uwanjani wakati Coastal Union wanafanya mazoezi siku moja kabla ya mchez huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENO KAKOLANYA AFUNGIWA NA FAINI JUU KWA MATUSI NA UGOMVI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top