• HABARI MPYA

  Sunday, December 03, 2023

  FIFA YAIFUTIA SIMBA SC ADHABU BAADA YA FEDHA ZA MAUZO YA SAKHO


  SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifutia klabu ya Simba adhabu ya kutofanya usajili hadi baada ya kuilipa klabu ya Teungueth ya Senegal sehemu ya mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho kwenda QRM ya Ufaransa.
  FIFA iliifungia Simba kufanya usajili hadi itakapoilipa klabu ya Teungueth sehemu ya mauzo ya mchezaji Pape Ousmane Sakho iliyemuuza US Quevilly-Rouen, ama US Quevilly, au QRM ya Ufaransa.
  Winga huyo wa kushoto mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na Simba SC Agosti mwaka 2021 akitokea Teungueth FC ya kwao, Senegal na baada ya misimu miwili mizuri akaondoka Msimbazi kwenda QRM inayoshiriki Ligi ya pili kwa ukubwa nchini Ufaransa, Ligue 2.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FIFA YAIFUTIA SIMBA SC ADHABU BAADA YA FEDHA ZA MAUZO YA SAKHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top