// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZIZ KI APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 4-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZIZ KI APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 4-1 CHAMAZI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Saturday, December 16, 2023

  AZIZ KI APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 4-1 CHAMAZI


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mtibwa Sugar leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga leo yamefungwa na Mburkinabe, kiungo Stephane Aziz Ki mawili, la kwanza kwa penalti dakika ya 45 na ushei na la pili dakika ya 65, mengine mshambulaji Mzambia Kennedy Musonda dakika ya 76 na winga Muafrika Kusini, Mahlatsi 'Skudu' Makudubela dakika ya 83.
  Bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 90 na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 10, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
  Hali inazidi kuwa mbaya kwa Mtibwa Sugar kwa baada ya kichapo cha leo, kwani wanendelea kushika mkia wakiwa na pointi tano kufuatia kushuka dimbani mara 13.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZIZ KI APIGA MBILI YANGA SC YAICHAPA MTIBWA SUGAR 4-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top