• HABARI MPYA

  Saturday, December 02, 2023

  KEN GOLD YAICHAPA TMA 2-0 NA KUPANDA KILELENI CHAMPIONSHIP


  WENYEJI, Ken Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya TMA katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Ushindi huo unawafanya 'Wachimba Dhahabu' hao, Ken Gold wafikishe pointi 29 katika mchezo wa 13 na kuendelea kuongoza Ligi ya NBC Championship kwa pointi tatu zaidi ya ndugu zao, Mbeya Kwanza ambao hata hivyo wana mechi moja mkononi na keshokutwa wanacheza na Pan Africans Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.   
  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship leo, Mbuni imeshinda 2-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Ruvu Shooting imechawa 1-0 na Cosmopolitan Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Transit Camp imetoa sare ya 1-1 na Stand United Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Kesho kutakuwa na mechi tatu za kukamilisha mzunguko wa 13; Fountain Gate Tallent dhidi ya Pamba Uwanja Jamhuri mjini Morogoro, Green Warriors dhidi ya Biashara United Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na keshokutwa ni Pan Africans dhidi ya Mbeya Kwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KEN GOLD YAICHAPA TMA 2-0 NA KUPANDA KILELENI CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top