• HABARI MPYA

  Sunday, December 10, 2023

  ASTON YAISHUGHULIKIA NA ARSENAL PIA, UTARATIBU ULE ULE, 1-0


  TIMU ya Aston Villa usiku wa jana imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Bao pekee la Aston Villa limefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Scotland, John McGinn dakika ya saba tu akimalizia pasi ya winga Mjamaica, Leon Bailey ambaye alifunga bao pekee la timu hiyo kwenye ushindi wa 1-0 pia dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City Desemba 6 hapo hapo Villa Park.
  Kwa ushindi huo, Aston Villa inafikisha pointi 35 na kusogea nafasi ya tatu ikizidiwa pointi moja tu na Arsenal na wote wakiwa nyuma ya Liverpool inayoongoza kwa pointi zake 37 baada ya wote kucheza mechi 16.
  Mabingwa watetezi, Manchester City sasa wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 30 za mechi 15 na leo watakuwa wageni wa Luton Town pale Kenilworth Road, Luton, Bedfordshire. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ASTON YAISHUGHULIKIA NA ARSENAL PIA, UTARATIBU ULE ULE, 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top