• HABARI MPYA

  Thursday, December 07, 2023

  AZAM FC YAENDELEZA DOZI YA ‘TANO TANO’, LEO ILIKUWA ZAMU YA KMC


  TIMU ya Azam FC imeendeleza dozi ‘Tano Tano’ baada ya kuichapa KMC mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo mawili, dakika ya 23 na 51, beki Ismail Gambo aliyejifunga dakika ya 43, winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 55 na kiungo mzawa, Feisal Salum dakika ya 60.
  Ushindi huo unawafanya Azam FC wafikishe pointi 25 katika mchezo wa 11 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu wakiwazidi pointi moja Mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao KMC baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 19 za mechi 12 nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAENDELEZA DOZI YA ‘TANO TANO’, LEO ILIKUWA ZAMU YA KMC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top