• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2023

  PIGO AZAM FC AHAMADA NAYE APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU


  KLABU ya Azam FC imepata pigo kubwa baada ya kipa wake Mcomoro, Ali Ahamada kuumia na kufanya sasa ibakiwe na kipa wa tatu pekee Zuberi Foba Masoud (21), zao la timu za vijana.
  Tayari Ahamada (32), amesafirishwa usiku wa kuamkia leo naye kwenda Jijini Cape Town, Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi wa goti lake la mguu wa kushoto aliloumia katika Hospitali ya Vincent Pallotti.
  Kipa huyo raia wa Ufaransa, alipata maumivu hayo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya KMC ambao Azam FC ilishinda 5-0 Desemba 7 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
  Hata hivyo, baada ya matibabu ya awali, Ahamada alipata nafuu na kumudu kucheza mchezo uliofuata dhidi ya JKT Tanzania Desemba 11, ambao Azam FC ilishinda 2-1, kabla ya maumivu hayo kuzidi hadi kusafirishwa Afrika Kusini kwa matibabu.
  Huyo anakuwa kipa wa pili wa Azam FC kuumia hadi kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu baada ya Mghana Iddrisu Abdulai (26), aliyefarishwa jana tu kufanyiwa uchunguzi zaidi wa maymivu ya bega lake la mkono wa kushoto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO AZAM FC AHAMADA NAYE APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top