• HABARI MPYA

  Friday, December 15, 2023

  SIMBA SC YAIKUNG’UTA KAGERA SUGAR 3-0 UWANJA WA UHURU


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 45 kwa penalti, Mmali Sadio Kanoute dakika ya 75 na mshambuliaji na Nahodha, John Raphael Bocco dakika ya 90 na ushei.
  Ushindi huo unaifanya Simba ifikishe pointi 22, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi tisa na wote wapo nyuma ya Azam FC yenye pointi 28 za mechi 12.
  Kwa upande wa Kagera Sugar baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 13 za mechi 12 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIKUNG’UTA KAGERA SUGAR 3-0 UWANJA WA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top