• HABARI MPYA

  Tuesday, December 05, 2023

  TWIGA STARS YAFUZU WAFCON LICHA YA KUCHAPWA 2-0 TOGO LEO


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (WAFCON) mwakani nchini Morocco licha ya kufungwa 2-0 na wenyeji, Togo leo Uwanja wa Kegue Jijini Lome.
  Katika mchezo huo marudiano Raundi ya Pili na ya mwisho ya kufuzu mabao yote ya Togo yalipatikana dakika 15 za mwisho na kwa matokeo hayo Twiga Stars inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 3-2, kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita.
  Mabao ya Twiga Stars katika mchezo wa kwanza Twiga Stars uliofanyika Alhamisi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam yalifungwa na mshambuliaji wa Besiktas ya Uturuki, Opa Clement mawili, dakika ya 45 na ushei kwa penalti na dakika ya 81, huku lingine Yawa Konou wa Togo akijifunga dakika ya 57.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YAFUZU WAFCON LICHA YA KUCHAPWA 2-0 TOGO LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top