• HABARI MPYA

    Tuesday, June 01, 2021

    AGUERO ATAMBULISHWA BARCELONA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI

    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina, Sergio Aguero ametambulishwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Barcelona kufuatia kusaini mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru kufuatia kuondoka Manchester City.
    Nyota huyo anayefikisha umri wa miaka 33 kesho, aliichezea kwa mara ya mwisho Man City Jumamos iliyopita katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikichapwa 1-0 na Chelsea nchini Ureno.
    Aguero alijiunga na Man City akitokea Atletico Madrid mwaka 2011 na kuifungia klabu hiyo mabao 260 akiiwezesha kushinda mataji matano ya Ligi Kuu England, moja la FA Cup na sita ya Kombe la Ligi.


    Kisoka Aguero, aliibukia Independiente ya kwao, Argentina kabla ya kuhamia Atletico mwaka 2006, ambako alifanikiwa kushinda taji la where he won the Europa League mwaka 2010.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AGUERO ATAMBULISHWA BARCELONA BAADA YA KUSAINI MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top